HISTORIA YA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE

Hayati Edward Moringe Sokoine alizaliwa Agosti 1, 1938 kitongoji cha Kilasho Kijiji cha Emairete Monduli Juu. Kwa wazazi wake, Baba Sokoine Ole Severe na Mama Napelel Sinyati Noomayaki -  Sokoine. Katika Familia yao walikuwa watoto watano. Yeye alikuwa wa tatu kwenye familia.

Kuzaliwa:                         01/08/1938

Kitongoji cha Kilasho, Kijiji cha Emairete, Monduli Juu.

Wazazi:

Elimu ya Msingi:

Elimu ya Sekondari:

Elimu ya Juu:

 

Baba Sokoine Ole Severe

Mama Napelel Sinyati Noomoyaki-Sokoine 1949-1953 Monduli Primary School

1953-1956 Monduli Middle School
1957-1958 Umbwe Secondary School

1962-1963 Mafunzo ya Maofisa Watendaji, Mzumbe

1963-1964 Akiwa Executive Officer alihudhuria mafunzo ya watumishi wa serikali za mitaa nchini Ujerumani

1981-1982 Alijiunga na Chuo Kikuu cha Belgrade, kusomea Uchumi wa Kijamaa alifuzu na kutunukiwa Diploma ya Juu.

1983 Chuo  Kiku  cha  Dar  es  Salaam    (UDSM)  kiliyatathmini  masomo  hayo
aliyoyafanya na kuyatambua kuwa ni sawa na shahada ya Bachelor of Arts

(BA) 1983-1984 Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuchukua masomo ya shahada ya juu ya sayansi ya siasa. Alifariki akiwa amebakiza sura moja kumaliza Thesis yake.

Siasa

Januari 1, 1961 Alijiunga na Chama cha TANU Februari 5, 1977 Alikuwa
mwanachama mwanzilishi wa CCM ilipoanzishwa 1977-1984 Mjumbe wa Kamati
Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM 1982 Katibu wa Tume ya Ulinzi na Usalama
Uongozi

1961-1962 Alijiunga   na   Serikali   za   Mitaa   kama   msaidizi   wa   Katibu  wa
Halmashauri ya Shirikisho la Masai (Masai Federal Council), baada ya muda
mfupi alipandishwa cheo kuwa Katibu wa Halmashauri ya Shirikisho la Masai.
1963 Baada ya masomo Mzumbe Training Centre, aliteuliwa kuwa Ofisa Mtendaji
Daraja la nne.

1965-1970 Mbunge wa Jimbo la Maasai (lililojumuisha majimbo ya sasa ya Ngorongoro, Longido, Monduli, Simanjiro na Kiteto).

1967 Aliteuliwa kuwa Waziri Mdogo (Naibu Waziri) wa Mawasiliano, Uchukuzi
na Kazi.

Novemba 1970 Aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu.

1970-1980 Mbunge  wa  Jimbo  la  Monduli     (lililojumuisha  majimbo  ya  sasa Monduli, Longido na Ngorongoro).

Februari 1972 Aliteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

13/02/1977 - 07/11/1980 Aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Novemba 1980 Alijiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu, kwa sababu za kiafya. 1980-
1984 Mbunge wa Jimbo la Monduli (Monduli na Longido ya sasa) Februari 24, 1983 Aliteuliwa kwa mara ya pili kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Nafasi aliyoishika hadi kifo chake Aprili 12, 1984

Marehemu Edward Moringe Sokoine alifariki dunia akiwa  Waziri  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge wa Jimbo la Monduli, Katibu wa Baraza la Ulinzi na Usalama, Mjumbe wa Kamti Kuu na Mjumbe  wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

Hayati Edward Moringe Sokoine alifariki akiwa na umri wa miaka 46 na aliacha
wajane wawili Mama Napono Sokoine na Mama Nekiteto Sokoine

sokoinepicture